KILIMO CHA ZAO LA VANILLA

Σχετικά έγγραφα
IDARA YA UTUMISHI WA MWALIMU


Kiswahili TE(C2).indd i 5/30/14 8:14 PM

Mradi wa Misitu ya Jamii MJUMITA (Lindi) Wilaya ya Lindi Vijijini na Manispaa ya Lindi, Mkoa wa Lindi, Tanzania

MUONGOZO RAHISI WA RAIA KUHUSU UCHAGUZI KATIKA MAMLAKA ZA SERIKALI ZA MITAA MWAKA 2014


i Kiswahili (TE) Class 1.indd i 5/30/14 8:07 PM

SURA YA 95 SHERIA YA MADAWA NA UZUIAJI WA USAFIRISHAJI WA MADAWA HARAMU SHERIA KUU MPANGILIO WA VIFUNGU SEHEMU YA 1 MASHARTI YA MWANZO

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA WIZARA YA AFYA NA USTAWI WA JAMII

Kuondoa Utata Uliyomo katika Tafauti ya Muandamo

IMAM MAHDI (A.S.) NI TUMAINI LA MATAIFA

Hadiyth Ya 71 Jikinge Na Moto Japo Kwa Tende Au Neno Jema )) :

Hadiyth Ya 131 Allaah Ameridhia Kuabudiwa, Kutokumshirikisha, Kuungana Na Anachukia Uvumi, Udadisi Na Kupoteza Mali ( )

Idghaam haiwezekani ikawa katika neno moja bali ni lazima nuwn saakinah au tanwiyn iweko mwisho wa neno la kwanza, na herufi inayoingizwa hiyo

Yaliyomo. ~ Ukurasa 3 ~

MATESO YA DHURIA YA MTUME

Hadiyth Ya 11 Daraja Za Iymaan Ni Sabini Na Kitu; Ya Juu Ni Tawhiyd, Na Ya Chini Kabisa Ni Kuondosha Taka Njiani

Ni kusimama katika neno lakini hata ukiunganisha yanayofuatia haiharibu maana. Ni lazima kusimama kwani kuunganisha na yanayofuatia kutaharibu maana.

Hadiyth Ya 61 Dunia Ni Kama Kivuli Anachokitumia Msafiri Kwa Muda Tu

Hadiyth Ya 111 Wanaume Na Wanawake Wasio Maharimu Wasitazamane Uchi Wala Wasilale Pamoja

Mafundisho Ya Madhehebu

AHLUL ~ KISAA. Mkusanyiko wa sifa na tarehe za Mtukufu Mtume (s.a.w.w.), Imamu Ali, Bibi Fatimah, Imamu Hassan na Imamu Hussein

25-Faharasa. Matamshi. Tamshi moja ni lafdhw. Iliyo na nguvu kabisa, inayodhaniwa kuwa sahihi kabisa, rai inayokubalika kabisa.

Hadiyth Ya 1 Allaah Hatazami Miili Wala Sura, Bali Anatazama Nyoyoni

Ummu Iyyaad Imepitiwa Na: Abu Abdillaah Muhammad Baawazir

ΛΕΞΙΚΟΝ ΕΛΛΗΝΟ-ΣΟΥΑΧΙΛΙ

05- Fadhila Za Umrah Na Hajj

2742/ 207/ / «&»

ΠΡΟΣΚΛΗΣΗ ΕΚΔΗΛΩΣΗΣ ΕΝΔΙΑΦΕΡΟΝΤΟΣ

( ) 1995.» 3 ( ). 10 ( ) ( ) 1986, ( ) (1) 3,, ( ),,,,».,,,

,+ 2 1ntr0du~a0 TABLE OF CONTENTS. a * 4. LT\,? .fi T? PAGE. n - q;.;.+e Afos ao carbono. Conepxakiue. CTpa~uqa ~Zgina Ukuras a

Γίτσα Σοντζόγλου-Κοτταρίδη. Η ΤΡΙΤΗ ΗΛΙΚΙΑ: ΜΥΘΟΣ ΚΑΙ ΠΡΑΓΜΑΤΙΚΟΤΗΤΑ** Σκέψεις για μια επιστημονική έρευνα

Ni hamzah inayotamkwa katika neno na haitamkwi (hutoweka) wakati wa kuunganisha na neno la nyuma yake.

Ε.Ε. Π α ρ.ι(i), Α ρ.4325, 30/3/2012 Ο ΠΕΡΙ ΔΑΣΩΝ ΝΟΜΟΣ ΚΑΤΑΤΑΞΗ ΑΡΘΡΩΝ

ΑΣΚΗΣΕΙΣ ΣΤΙΣ ΕΞΙΣΩΣΕΙΣ

ί α α I. Β α μ α π α μ α μ π φα α υ α υ αμ α ία ( α. μ3) : ία & α μα μα - αμ υ α ) α α Θ π μα α 79 (55) * 107

ΕΛΤΙΟ ΤΥΠΟΥ. ΕΙΚΤΗΣ ΤΙΜΩΝ ΥΛΙΚΩΝ ΚΑΤΑΣΚΕΥΗΣ ΝΕΩΝ ΚΤΙΡΙΩΝ ΚΑΤΟΙΚΙΩΝ: εκέµβριος 2015 (2010=100,0)

, &

ΚΑΝΟΝΙΣΜΟΣ (EE) 2019/1238 ΤΟΥ ΕΥΡΩΠΑΪΚΟΥ ΚΟΙΝΟΒΟΥΛΙΟΥ ΚΑΙ ΤΟΥ ΣΥΜΒΟΥΛΙΟΥ

ΔΙΑΚΗΡΥΞΗ Ο ΑΝΤΙΔΗΜΑΡΧΟΣ ΟΙΚΟΝΟΜΙΚΩΝ ΔΗΜΟΥ ΙΩΑΝΝΙΤΩΝ. Ιωάννινα Α.Π /6638

A. Αὐτοτελεῖς δημοσιεύσεις:

ΑΞΙΟΛΟΓΗΣΗ ΤΗΣ ΕΡΓΟΛΑΒΙΚΗΣ ΚΑΤΟΙΚΙΑΣ ΩΣ ΕΠΕΝΔΥΣΗ

Νόµοςπεριοδικότητας του Moseley:Η χηµική συµπεριφορά (οι ιδιότητες) των στοιχείων είναι περιοδική συνάρτηση του ατοµικού τους αριθµού.

Αριθμός αποφάσεως 5928/2010 ΤΟ ΠΟΛΥΜΕΛΕΣ ΠΡΩΤΟΔΙΚΕΙΟ ΠΕΙΡΑΙΑ (Διαδικασία Εκούσιας Δικαιοδοσίας)

ΕΛΛΗΝΙΚΗ ΔΗΜΟΚΡΑΤΙΑ. 18:00-20:00 Π. αμφ, 002, 201, 202, 203, ΔΕΧΡΗ16-ΔΙΑΧΕΙΡΙΣΗ ΚΙΝΔΥΝΟΥ Α - Ω ΔΕΧΡΗ16

ΛΙΓΕΣ ΣΚΕΨΕΙΣ ΓΙΑ ΤΗ ΖΩΓΡΑΦΙΚΗ ΤΟΥ ΓΙΑΝΝΗ ΣΤΕΦΑΝΑΚΙ

Για κάθε διδακτική ενότητα ακολουθείται η λεγόμενη τετραμερής πορεία, χωρίζεται δηλαδή η διδασκαλία σε τέσσερα κύρια στάδια.

Δύναμη των ελληνικών εμπορικών πλοίων, 100 ΚΟΧ και άνω Αύγουστος 2007

ΔΙΕΡΕΥΝΗΣΗ ΛΕΙΤΟΥΡΓΙΑΣ ΟΡΓΑΝΩΜΕΝΩΝ ΧΩΡΩΝ ΣΤΑΘΜΕΥΣΗΣ ΔΙΚΥΚΛΩΝ ΣΤΟ ΚΕΝΤΡΟ ΤΗΣ ΘΕΣΣΑΛΟΝΙΚΗΣ

ΤΜΗΜΑ ΧΡΗΜΑΤΟΟΙΚΟΝΟΜΙΚΗΣ ΚΑΙ ΤΡΑΠΕΖΙΚΗΣ ΔΙΟΙΚΗΤΙΚΗΣ Πειραιάς:22/2/2013

Μοντελοποίηση Στατικού Ηλεκτρισμού Νικόλας Νικολάου Καθηγητής φυσικής Λύκειο Αγίου Αντωνίου

ΝΟΜΟΣ ΤΗΣ ΠΕΡΙΟ ΙΚΟΤΗΤΑΣ : Οι ιδιότητες των χηµικών στοιχείων είναι περιοδική συνάρτηση του ατοµικού τους αριθµού.

HONDA. Έτος κατασκευής

ΣΧΟΛΗ ΕΠΙΣΤΗΜΩΝ ΙΟΙΚΗΣΗΣ ΕΠΙΧΕΙΡΗΣΕΩΝ ΤΜΗΜΑ ΛΟΓΙΣΤΙΚΗΣ ΚΑΙ ΧΡΗΜΑΤΟΟΙΚΟΝΟΜΙΚΗΣ

ΚΑΝΟΝΙΣΜΟΣ (ΕΕ) 2019/1243 ΤΟΥ ΕΥΡΩΠΑΪΚΟΥ ΚΟΙΝΟΒΟΥΛΙΟΥ ΚΑΙ ΤΟΥ ΣΥΜΒΟΥΛΙΟΥ

στο σχέδιο νόµου «Κύρωση του Πρωτοκόλλου µεταξύ το οποίο τροποποιεί τη Σύµβαση µεταξύ της Ελληνικής Δηµοκρατίας και της Ελβετικής Συνοµοσπονδίας

Διαχρονικές Τάσεις Δεικτών Ανθρώπινου Δυναμικού στην Κύπρο: Συμμετοχή και Προσφορά στην Αγορά Εργασίας

ΓΕΝΙΚΟΙ ΟΡΟΙ ΚΑΙ ΠΡΟΫΠΟΘΕΣΕΙΣ. (σε ισχύ από την 1 η Φεβρουαρίου 2014)

ΠΡΟΫΠΟΘΕΣΕΙΣ ΕΙΣΟΔΟΥ ΚΑΙ ΓΕΝΙΚΟΙ ΟΡΟΙ ΧΡΗΣΗΣ ΤΟΥ ΔΙΚΤΥΑΚΟΥ ΤΟΠΟΥ

ΕΦΗΜΕΡΙΣ ΤΗΣ ΚΥΒΕΡΝΗΣΕΩΣ

K r i t i k i P u b l i s h i n g - d r a f t

ΤΟΠΙΚΟ ΣΧΕΔΙΟ ΔΙΑΧΕΙΡΙΣΗΣ ΑΠΟΒΛΗΤΩΝ ΔΗΜΟΥ ΗΡΑΚΛΕΙΟΥ

ΑΠΟΦΑΣΗ ΑΡΙΘ. 544/VII/2012* Η ΕΠΙΤΡΟΠΗ ΑΝΤΑΓΩΝΙΣΜΟΥ ΣΕ TMHMA

Φαρμακευτική Τεχνολογία ΙΙ

ΕΛΛΗΝΙΚΗ ΔΗΜΟΚΡΑΤΙΑ. Πειραιάς 16/05/2013 ΩΡΕΣ ΑΙΘΟΥΣΕΣ ΕΞ.-ΤΥΠΟΣ ΜΑΘΗΜΑ ΒΑΡΔΙΑ ΚΩΔΙΚΟΣ ΕΞΕΤΑΣΤΕΣ. Δευτέρα, 10/06/2013

25770 ΕΦΗΜΕΡΙΣ ΤΗΣ ΚΥΒΕΡΝΗΣΕΩΣ (ΤΕΥΧΟΣ ΔΕΥΤΕΡΟ)

ΤΕΧΝΟΛΟΓΙΚΟ ΕΚΠΑΙΔΕΥΤΙΚΟ ΙΔΡΥΜΑ ΚΑΒΑΛΑΣ ΣΧΟΛΗ ΔΙΟΙΚΗΣΗΣ & ΟΙΚΟΝΟΜΙΑΣ ΤΜΗΜΑ ΛΟΓΙΣΤΙΚΗΣ

ΕΚΘΕΤΙΚΗ ΚΑΙ ΛΟΓΑΡΙΘΜΙΚΗ ΣΥΝΑΡΤΗΣΗ ΣΩΣΤΑ ΛΑΘΟΣ

Ο ΠΕΡΙ ΤΗΣ ΕΠΙΒΟΛΗΣ ΠΕΡΙΟΡΙΣΤΙΚΩΝ ΜΕΤΡΩΝ ΣΤΙΣ ΣΥΝΑΛΛΑΓΕΣ ΣΕ ΠΕΡΙΠΤΩΣΗ ΕΚΤΑΚΤΗΣ ΑΝΑΓΚΗΣ ΝΟΜΟΣ ΤΟΥ Διάταγμα δυνάμει των άρθρων 4 και 5

ΥΠΟΥΡΓΕΙΟ ΠΑΙ ΕΙΑΣ ΚΑΙ ΠΟΛΙΤΙΣΜΟΥ ΙΕΥΘΥΝΣΗ ΑΝΩΤΕΡΗΣ ΚΑΙ ΑΝΩΤΑΤΗΣ ΕΚΠΑΙ ΕΥΣΗΣ

H Εξωτερική Αξιολόγηση στο ΑΠΘ

Language, Mobile Phones and Internet: A Study of SMS Texting, , IM and SNS Chats in Computer Mediated Communication (CMC) in Kenya

ΣΑΟΡΖΠ ΓΗΘΑΗΥΚΑΡΥΛ ΘΑΗ ΞΝΣΟΔΥΠΔΥΛ ΡΝ ΓΖΚΝΡΖ. Απφθαζε Γεκνηηθνχ Ππκβνπιίνπ ππ αξηζκ. 157/2011

ΔΙΚΤΥΟ «ΓΑΣΤΡΟΝΟΜΙΚΕΣ ΠΕΡΙΠΛΑΝΗΣΕΙΣ ΚΑΙ Ο ΠΟΛΙΤΙΣΜΟΣ ΤΩΝ ΓΕΥΣΕΩΝ» ΑΝΑΛΥΤΙΚΟ ΤΕΥΧΟΣ ΠΡΟΚΗΡΥΞΗΣ ΠΡΟΧΕΙΡΟΥ ΑΝΟΙΧΤΟΥ ΔΙΑΓΩΝΙΣΜΟΥ ΔΡΑΣΗΣ 1

Τα δικαιώματά σας κοινωνικής ασφάλισης

Α Π Ο Φ Α Σ Ι Ζ Ο Υ Μ Ε. A. Ορίζουµε αναπληρωτές Προϊσταµένους των νεοσύστατων Τµηµάτων, τους παρακάτω υπαλλήλους:

- International Scientific Electronic Journal, Issue 1, 2004 Department of Cultural Technology and Communication University of the Aegean

Αθήνα, Α.Π. Φ80000/οικ.59819/1961

Στοιχεία και έγγραφα που απαιτούνται για την εγγραφή στο ΓΕΜΗ

Ασκήσεις. ι) α α ιι) α α ΠΡΟΣΘΕΣΗ - ΑΦΑΙΡΕΣΗ ΡΗΤΩΝ

(2), ,. 1).

ΚΕΝΤΡΟ ΠΡΟΓΡΑΜΜΑΤΙΣΜΟΥ ΚΑΙ ΟΙΚΟΝΟΜΙΚΩΝ ΕΡΕΥΝΩΝ ΑΜΕΡΙΚΗΣ 11, ΑΘΗΝΑ Τ.Κ , Τηλ Fax


3. α) = + 13 β) = + 10 γ) = + 9 δ) = = 0-3 = - 2 = - 1 = = + 1 = + 2 =

Ε.Σ.Π.Α και Τοπική Αυτοδιοίκηση. Οι δυνατότητες ένταξης έργων και δράσεων της Τ.Α. στα Επιχειρησιακά Προγράμματα

Η ΕΞΕΛΙΞΗ ΤΟΥ ΚΛΑΔΟΥ ΤΡΟΦΙΜΩΝ ΣΕ ΠΕΡΙΟΔΟ ΚΡΙΣΗΣ: Η ΠΕΡΙΠΤΩΣΗ ΤΗΣ ΕΠΙΧΕΙΡΗΣΗΣ ΕΒΡΟΦΑΡΜΑ Α. Β. Ε. Ε.

Να βρείτε ποιες από τις παρακάτω συναρτήσεις είναι γνησίως αύξουσες και ποιες γνησίως φθίνουσες. i) f(x) = 1 x. ii) f(x) = 2ln(x 2) 1 = (, 1] 1 x

Μεταϖτυχιακή Εργασία. Εκτίµηση εϖικινδυνότητας της ϖοιότητας του νερού του δικτύου ύδρευσης του ήµου Ηρακλείου του Νοµού Ηρακλείου Κρήτης

Οργάωνση του Περιφερικού Νευρικού Συστήµατος λκλλκλκλλκκκκ

Συμβούλιο της Ευρωπαϊκής Ένωσης Βρυξέλλες, 7 Μαρτίου 2017 (OR. en)

ΑΡΧΑΙΑ ΕΛΛΗΝΙΚΗ ΓΛΩΣΣΑ ΚΑΙ ΓΡΑΜΜΑΤΕΙΑ Α ΤΑΞΗ ΗΜΕΡΗΣΙΟΥ ΓΕΝΙΚΟΥ ΛΥΚΕΙΟΥ ΚΑΙ Α, Β ΤΑΞΕΙΣ ΕΣΠΕΡΙΝΟΥ ΓΕΝΙΚΟΥ ΛΥΚΕΙΟΥ

ΠΑΡΑΡΤΗΜΑ ΠΡΩΤΟ ΤΗΣ ΕΠΙΣΗΜΗΣ ΕΦΗΜΕΡΙΔΑΣ ΤΗΣ ΔΗΜΟΚΡΑΤΙΑΣ Αρ της 6ης ΑΠΡΙΑΙΟΥ 1998 ΝΟΜΟΘΕΣΙΑ ΜΕΡΟΣ Ι

«ΣΧΕΔΙΑΣΜΟΣ ΘΕΡΜΙΚΟΥ ΗΛΙΑΚΟΥ ΣΥΣΤΗΜΑΤΟΣ ΓΙΑ ΤΑ ΜΕΤΕΩΡΟΛΟΓΙΚΑ ΔΕΔΟΜΕΝΑ ΤΗΣ ΠΑΤΡΑΣ»

ΠΑΡΑΡΤΗΜΑ Α ΤΗΣ 14/2015 ΜΕΛΕΤΗΣ ΤΕΧΝΙΚΗΣ ΥΠΗΡΕΣΙΑΣ ΔΗΜΟΥ ΑΛΜΩΠΙΑΣ

ΕΙΣΑΓΩΓΗ ΣΤHN. Δρ. Α. ΤΖΑΝΗ

lujo οό ΚΕΦΑΛΑΙΟ A Κυριότητα ακινήτου /. Γενικά 2. Κυριότψα βεβεφημένη με περιορισμένα εμπράγματα δικαιώματα 3. Μετακλητή κυριότψα

ΣΕΝΑΡΙΑ. Η Πρώτη Αναγνώριση

Π Α Ν Α Γ Ι Ω Τ Η Π Α Ν Ο Π Ο Υ Λ Ο Υ ΣΙΩΝΙΣΜΟΣ ΤΑ ΣΧΕΔΙΑ ΜΙΑΣ ΜΑΚΡΟΧΡΟΝΙΑΣ ΣΥΝΩΜΟΣΙΑΣ. «Επί των ποταμών Βαβυλώνος εκεί εκαθίσαμεν

ΔΗΛΩΣΗ περιουσιακής κατάστασης έτους 2014 του Ν.3213 / 2003 (ΦΕΚ 309/A/ ) όπως έχει τροποποιηθεί και ισχύει

ΕΘΝΙΚΟ ΜΕΤΣΟΒΙΟ ΠΟΛΥΤΕΧΝΕΙΟ ΣΧΟΛΗ ΑΓΡΟΝΟΜΩΝ ΤΟΠΟΓΡΑΦΩΝ ΜΗΧΑΝΙΚΩΝ ΤΟΜΕΑΣ ΓΕΩΓΡΑΦΙΑΣ & ΠΕΡΙΦΕΡΕΙΑΚΟΥ ΣΧΕΔΙΑΣΜΟΥ

Transcript:

KILIMO CHA ZAO LA VANILLA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA WIZARA YA KILIMO, CHAKULA NA USHIRIKA

IDARA YA MAENDELEO YA MAZAO Sehemu ya Uendelezaji wa Mazao KILIMO CHA ZAO LA VANILLA Kimetolewa na Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Wizara ya Kilimo, Chakula na Ushirika Idara ya Maendeleo ya Mazao Sehemu ya Uendelezaji wa Mazao S.L.P. 9192 Dar es Salaam - Tanzania Simu: +255 22 2864899 Barua Pepe: cps@kilimo.go.tz Wizara ya Kilimo na Chakula Haki zote zimehifadhiwa Toleo la Kwanza 2006 Kimechapishwa na: Colour Print (T) Ltd. 4 Kilimo cha Zao la Vanilla

DIBAJI Vanilla ni zao la viungo na moja ya mazao yasiyo ya asili ya kibiashara. Zao hili kwa sasa lina thamani na uhitaji mkubwa katika soko, hivyo wakulima wengi wameonyesha ari ya kulima zao hili na wengi wameanza kulima bila uelewa wa kutosha. Katika jitihada za kuwawezesha wakulima kuongeza kipato, kupunguza umaskini na kuinua uchumi, Wizara imeamua kuandaa kitabu hiki cha muongozo wa uzalishaji wa zao la vanilla. Kitabu hiki kimekusudiwa kutumika na maafisa ugani na wakulima hapa nchini kwa lengo la kuongeza uzalishaji na ubora wa zao hili. Kitabu kina sehemu kuu tatu. Sehemu ya kwanza inazungumzia juu ya umbile la mmea wa vanilla na mazingira yanayofaa katika kustawisha zao hilo. Sehemu ya pili inahusu uzalishaji wa vanilla katika vipengele vya upandaji, utunzaji wa mimea shambani, uchavushaji na udhibiti wa magonjwa, wadudu na wanyama waharibifu. Sehemu ya tatu inalenga katika uvunaji na sehemu ya nne katika ukaushaji na uhifadhi wa zao. Kilimo cha Zao la Vanilla i

ii Kilimo cha Zao la Vanilla

SHUKRANI Wizara ya Kilimo, Chakula na Ushirika inapenda kuwashukuru wadau mbalimbali waliohusika katika kutoa mchango wao aidha kwa taarifa au majadiliano ambayo yamesaidia sana katika kufanikisha uandishi wa kitabu hiki. Shukrani za pekee zinatolewa kwa wataalamu wa Wizara ya Kilimo, Chakula na Ushirika waliohusika katika uandishi na uhariri wa kitabu hiki, wakulima wa zao la Vanilla wa Mkoa wa Kagera waliohojiwa pamoja na Chama cha Maendeleo Ya Wakulima (MAYAWA) kilichopo Mkoani Kagera, kwa taarifa mbalimbali zilizosaidia kufanikisha uandishi wa kitabu hiki. Kilimo cha Zao la Vanilla iii

iv Kilimo cha Zao la Vanilla

UTANGULIZI Zao la vanilla ni moja ya zao la viungo ambalo asili yake ni Kusini Mashariki ya Mexico na sehemu nyingine za Amerika ya Kati. Vanilla hulimwa katika nchi mbalimbali duniani. Nchi zinazolima kwa wingi ni pamoja na Madagascar, Comoro, Tahiti, Uganda, India na nchi nyingine za Amerika ya Kati. Tanzania ni miongoni mwa nchi zinazolima vanilla katika Afrika. Zao hili lilianza kuingia nchini kutoka Uganda mnamo mwaka 1954 kupitia kwa mkulima mmoja wa kijiji cha Kiilima wilaya ya Bukoba Vijijini. Vanilla imeanza kulimwa kibiashara hasa katika mkoa wa Kagera mwaka wa 1992. Katika mkoa wa Kagera, kilimo cha Vanilla kimehamasishwa zaidi na Chama cha Maendeleo Ya Wakulima kinachofahamika kama MAYAWA. Chama hiki kimekuwa kikihimiza uzalishaji na usindikaji wa Vanilla ambayo huuzwa kupitia kampuni zilizopo Uganda. Mmea wa Vanilla huzaa maharage ( mapodo) ambayo hukaushwa kwa njia maalum inayowezesha kupatikana kwa Kemikali inayoitwa Vanillini. Kemikali hiyo hutumika katika kuongeza laadha na herufu nzuri kwenye vyakula na vinywaji mbalimbali. Pia hutumika katika viwanda vinvyotengeneza Vipodozi na Dawa za matibabu ya binadamu. Kwa matumizi ya kawaida, Vanilla huweza kutumika katika vinywaji kama Chai, Maziwa na mapishi ya Vyakula mbalimbali. Maeneo mengine ya Tanzania yanayoweza kulima zao la vanilla ni pamoja na wilaya za Mbeya Vijijini, Tukuyu, Morogoro Vijijini, Mvomero, Muheza, Arumeru na Ukerewe. Kilimo cha Zao la Vanilla v

vi Kilimo cha Zao la Vanilla

YALIYOMO Dibaji...(i) Shukrani...(iii) Utangulizi...(v) Orodha ya Vielelezo...(viii) SURA YA KWANZA Umbile la mmea na mazingira yanayofaa...1 SURA YA PILI Uzalishaji wa Vanilla...5 SURA YA TATU Uvunaji...21 SURA YA NNE Ukaushaji na uhifadhi...23 Kilimo cha Zao la Vanilla vii

ORODHA YA VIELELEZO Picha Na. 1: Mmea wa Vanilla...1 Picha Na. 2: Rando linalofaa kupandwa...9 Picha Na. 3: Jinsi ya kupanda rando...10 Picha Na. 4: Ua lililochanua...14 Picha Na. 5: Jinsi ya kuchavusha...15 Mchoro Na. 1: Mpangilio wa mashimo...6 Mchoro Na. 2: Jinsi ya kupanda miega...8 Mchoro Na. 3: Jinsi ya kuningíiniza rando...12 Mchoro Na. 4: Jinsi ya kulisha rando...13 viii Kilimo cha Zao la Vanilla

SURA YA KWANZA UMBILE LA MMEA NA MAZINGIRA YANAYOFAA Mmea wa Vanilla upo katika familia ya Okidi (Orchidaceae) ambayo ina genera zipatazo 700. Kati ya hizo, genera moja itwaayo vanilla ndio yenye umuhimu wa kiuchumi. Genera ya Vanilla ina aina au jamii zipatazo 110, kati ya hizo ni mbili ambazo huzalishwa kibiashara. Aina hizo ni Bourbon ya nchini Mexico na Tahitian ya visiwa vya Tahiti. 1.1 Umbile la Mmea wa Vanilla Mmea wa Vanilla ni rando teke linalotambaa ambalo ni la kudumu. Mmea huu hukua na kutambaa katika mti mwingine hadi kufikia urefu wa mita 10 hadi 15 na zaidi kutegemea na mazingira. Picha Na 1: Mmea wa Vanilla Kilimo cha Zao la Vanilla 1

1.1.1 Mizizi Mizizi ya mmea huu ni mirefu ina rangi nyeupe, myembamba yenye kipenyo cha milimita mbili. Mizizi hutokea kwenye fundo la shina lililo ndani ya udongo na hutambaa sambamba na tabaka la udongo wenye rutuba. Pia hutokea katika vifundo vya shina sambamba na majani ambayo hujishikiza katika miti ya kuegemea. 1.1.2 Shina Shina la vanilla lina rangi ya kijani, refu lenye vifundo na kipenyo cha sentimeta moja hadi mbili. Nafasi kati ya fundo na fundo ni sentimita tano (5) hadi 15. 1.1.3 Majani Majani yana rangi ya kijani iliyokolea, yenye umbile la bapa, lenye ncha, nene na kubwa. Huota kwa kupishana katika shina, yana urefu wa sentimita nane hadi 25 na upana wa sentimita mbili hadi nane, na yana rangi ya kijani iliyokolea. 1.1.4 Maua Maua yana rangi mchanganyiko wa kijani na njano na kipenyo cha sentimita 10. Huota katika vifungu vyenye maua kati ya 18 hadi 30. 1.1.5 Matunda Matunda yana umbile la podo la harage lenye rangi ya kijani likiwa changa. Hubadilika kuwa rangi ya njano, hatimaye kahawia kadri linavyokomaa. Podo lina urefu wa sentmeta 10 hadi 25, kipenyo cha sentimeta nane hadi 15 na lina mbegu ndogo sana ambazo huonekana linapokomaa. 1.2 Mazingira Yanayofaa katika Uzalishaji wa Zao la Vanilla Mmea wa vanilla una asili ya msituni hivyo huhitaji kuoteshwa katika sehemu yenye kivuli na mvua ya kutosha. Ili zao hili liweze kukua vizuri linahitaji mazingira yafuatayo: 2 Kilimo cha Zao la Vanilla

1.2.1 Mvua Mmea wa Vanilla huhitaji kiasi cha mvua cha milimita 1250 hadi 2500 kwa mwaka. Pia zao hili huhitaji kipindi cha miezi mawili cha ukame ili kuweza kusisisimka na kutoa vitumba vya maua. 1.2.2 Joto Zao hili hustawi vizuri katika maeneo yenye nyuzi joto 20 hadi 30 za Sentigredi. Pia huweza kustahimili nyuzi joto 32 za Sentigredi. Lakini hukua vizuri zaidi katika kiwango cha nyuzi joto 27 za Sentigredi. 1.2.3 Mwinuko Zao hili hustawi vizuri katika maeneo yenye mwinuko wa mita 0 hadi 600 kutoka usawa wa bahari. Pia hustawi katika maeneo yenye mwinuko unaofikia mita 1500 katika nchi za joto (tropiki). 1.2.4 Udongo Mmea wa vanilla una mizizi ambayo hutambaa katika sehemu ya juu ya udongo. Hivyo, huhitaji udongo mwepesi wa tifutifu, wenye rutuba ya kutosha na usiotuamisha maji. 1.2.5 Mwanga Mmea wa vanilla huathirika kwa jua na husababisha kuungua kwa majani, hivyo huhitaji kivuli cha asilimia 50 hadi 75 ili uweze kukua vizuri. Kivuli kinaweza kupatikana kwa kupanda miti au kwa kutengenezwa kitaalamu. Kilimo cha Zao la Vanilla 3

4 Kilimo cha Zao la Vanilla

SURA YA PILI UZALISHAJI WA ZAO LA VANILA Vanilla huzalishwa kwa kupandikiza marando moja kwa moja shambani au kwa kukuzwa kwanza kwenye kitalu na baadaye kupandikizwa shambani. Kabla ya kupanda inatakiwa kuzingatia yafuatayo: 2.1 Uchaguzi wa Shamba Shamba la kupanda vanilla inafaa liwe mahali pasipo na upepo mkali ili kuepuka kuanguka kwa miti ya kuegemea na kukatika kwa mimea. Ni muhimu kupanda miti ya kuzuia upepo ikiwa mahali hapo pana upepo mkali. Shamba hilo pia liwe na udongo usiotuamisha maji, mwepesi na ambao unaruhusu mizizi kupenya kwa urahisi. Aidha, shamba lisiwe na magugu mabaya (kwa mfano kwekwe/sangare) ambayo hulazimu kutumia jembe mara kwa mara wakati wa palizi. Kutumia jembe huweza kusababisha kukatika au kuharibu mizizi na kuhatarisha ukuaji wa mmea. 2.2 Utayarishaji wa Shamba Utayarishaji wa shamba huhusisha shughuli mbalimbali kama vile usafishaji wa shamba, utayarishaji wa mashimo na uwekaji wa mbolea. 2.2.1 Kusafisha Shamba Shamba lisafishwe kwa kulima, kungíoa visiki, magugu mabaya na kutifua hadi kina kisichopungua sentimita 30. 2.2.2 Kutayarisha Mashimo Mashimo yatayarishwe miezi miwili hadi mitatu sambamba na usafishaji wa shamba. Yawe na kina cha sentimita 30 na upana wa sentimita 60 hadi 90. Nafasi kati ya mstari na mstari iwe mita mbili na nusu hadi mita tatu na kati ya shimo na shimo iwe mita moja na nusu hadi mbili. Udongo wa juu utengwe na ule wa chini. Kilimo cha Zao la Vanilla 5

Mchoro Na 1: Mpangilio wa mashimo 2.2.3 Uwekaji wa Mbolea Mbolea za asili kama mboji, vunde au samadi ichanganywe vema na udongo wa juu na kujazwa kwenye shimo kwa kipimo cha debe moja hadi mbili kwa kila shimo. 2.3 Mifumo ya Upandaji Zao la vanilla huweza kupandwa shambani kwa kutumia mifumo mikuu mitatu ifuatayo: (i) Vanilla Pekee Mfumo huu unahusisha upandaji wa mmea wa vanilla na miti ya kuegemea tu ambayo hutoa kivuli kwa mimea. (ii) Vanilla na Migomba Mfumo huu unawezesha kuotesha vanilla katika shamba la migomba, ambapo rando hupandwa pamoja na mti wa kuegemea ndani ya shamba la migomba. 6 Kilimo cha Zao la Vanilla

(iii)vanilla na Miti ya Kivuli Katika mfumo huu vanilla huoteshwa katika shamba la miti ya kivuli, ambapo mmea hupandwa na miti ya kuegemea katikati ya miti ya kivuli. Kumbuka: Mfumo wa pili na wa tatu unapendekezwa zaidi kutokana na matokeo yake mazuri. 2.4 Upandaji wa Miti ya Kuegemea (miega) Miti ya kuegemea hupandwa miezi miwili hadi mitatu kabla ya kupanda rando la vanilla ili iweze kuchipua, kutoa kivuli na kuwa na uwezo wa kuhimili mimea. (i) Sifa za Miega Miti inayofaa kutumika kwa kuegemea iwe na sifa zifuatazo: Uwezo wa kukua haraka bila kuathiri mmea wa vanilla. Uwezo wa kutoa kivuli kinachofaa. Uwezo wa kuchipua haraka inapopunguzwa. Uwezo wa kuchipua matawi kwa chini ili kupandishia marando kwa urahisi. Uwezekano wa kuoteshwa kwa urahisi. Miti yenye sifa hizo ni pamoja na mibono (Jatropha carcus) na Gilirisidia. Miti mingine inayoweza kutumika kwa kivuli na kuegemea ni pamoja na Erythrina spp na Bauhania spp. (ii) Kupanda Miega ya Mibono Miti inayotumika zaidi katika mashamba ya vanilla ni jamii ya Jatropha. Miti hii huoteshwa kwa kutumia mbegu au kipande cha tawi kwa umbali wa sentimita 30 kutoka katika shimo la kupandia vanilla. Tawi la mbono lenye urefu wa sentimita 120 hadi 150 hupandwa katika kina cha sentimita10 hadi 15. Kilimo cha Zao la Vanilla 7

Mchoro Na 2:Jinsi ya kupanda miega 2.5 Upandaji wa Vanilla Mmea wa vanilla hupandwa mwanzoni mwa msimu wa mvua ili kuhakikisha upatikanaji wa unyevu ardhini. Hupandwa kwa kutumia rando lenye urefu wa kati ya sentimita 100 hadi 150 (futi tatu na nusu hadi tano) kutoka kwenye mmea unaokuwa vizuri, usio na magonjwa na wenye pingili ndefu. Rando lenye sifa hizo hukua haraka na kutoa maua mapema (miaka 2). Rando fupi halikui haraka na huchukua muda mrefu kutoa maua (miaka 2 Ω hadi 3). 2.5.1 Kutayarisha Marando Kata rando kwa kutumia kisu kikali kwa kufuata vipimo (sentimita 100 hadi 150). Ondoa majani matatu hadi matano katika sehemu ya chini ya rando itayofukiwa kwenye udongo. Ningíiniza rando lililokatwa kwenye kivuli kwa muda wa siku saba hadi 10 kabla ya kupanda ili kupunguza utomvu na kulipa nguvu ya kuchipua na kuhimili hali ya shambani. 8 Kilimo cha Zao la Vanilla

Picha Na 2: Rando linalofaa kupandwa 2.5.2 Jinsi ya Kupanda Upandaji wa vanilla hufanywa kwa kutumia hatua zifuatazo: Andaa nyasi kavu (matandazo) ambazo zitatumika mara baada ya kupanda. Tengeneza kifereji chenye kina cha sentimita 10 hadi 12 katikati ya shimo lenye mbolea lililokwisha tengenezwa. Laza sehemu ya rando iliyotolewa majani katika kifereji hicho, acha sehemu yenye majani juu ya ardhi. Fukia rando kwenye kifereji kwa udongo na gandamiza taratibu ili lishikamane na udongo. Funga sehemu ya juu ya rando kwa kutumia kamba katika umbile la nane kwenye mti wa kuegemea. Weka matandazo kuzunguka kila shina lililopandwa. Kumbuka: Utaratibu huu wa kupanda hutumika katika aina zote za mifumo ya kuzalisha vanilla, na hutofautiana kwa nafasi za upandaji kati ya mfumo mmoja na mwingine. Kilimo cha Zao la Vanilla 9

Shamba la vanilla pekee katika miaka ya mwanzoni, huweza kuchanganywa katikati ya mistari na mazao mengine ya muda mfupi kama mazao ya jamii ya mikunde. Picha Na 3: Jinsi ya kupanda marando 2.6 Utunzaji wa Shamba Vanilla huhitaji kutunzwa vizuri ili iweze kukua vizuri na kutoa mavuno yenye ubora wa hali ya juu. Huduma muhimu katika uzalishaji wa vanilla ni kama ifuatavyo: 2.6.1 Kutengeneza Kivuli Mmea wa vanilla huhitaji kivuli ili uweze kukua vizuri. Hivyo ni muhimu kupanda miti ya kivuli kabla ya kustawisha vanilla. Katika ukuaji wake kuanzia inapopandwa hadi inapokaribia kutoa maua huhitaji kivuli cha kutosha kinachoweza kuzuia jua kali na kuruhusu mwanga (asilimia 60 hadi 70). Kipindi cha kusisimua kivuli kipunguzwe zaidi na kufikia asilimia 55 hadi 50. Kivuli kitengenezwe kwa kupunguza matawi ya miti ya miega na ya kivuli ili kupata kivuli kinachofaa. 10 Kilimo cha Zao la Vanilla

Kumbuka: Kivuli kizito huathiri ukuaji wa mmea. 2.6.2 Kuweka Matandazo Utandazaji wa nyasi ni muhimu katika shamba la vanila kutokana na tabia ya ukuaji wa mizizi ambayo huota katika kina cha sentimita 5 hadi 10, hivyo huhitaji kulindwa isiharibiwe. Matandazo yawekwe kuzunguka mashina ya mimea ili kuhifadhi unyevu, kuzuia uotaji wa magugu, na kulinda mizizi isiharibiwe wakati wa palizi. Kumbuka: Matandazo yawe makavu na yasiwe na mbegu za magugu. 2.6.3 Palizi Palizi hufanyika wakati wowote magugu yanapoota shambani. Inashauriwa kufanya palizi kabla ya mvua kunyesha ili mmea uweze kutumia maji ya mvua ipasavyo. Palizi ifanyike wakati wowote magugu yanapoota shambani, kwa kungíoa magugu kutumia mikono ili kuepuka kujeruhi mizizi jembe linapotumika. 2.6.4 Kuningíiniza Marando Mmea wa vanilla uliokua vizuri huota matawi (marando) mengi na marefu. Marando hayo huelekezwa kwenye matawi ya miti ya kuegemea na kuningíinizwa. Rando linapofikia urefu wa sentimita 150 hadi 180 liningíinizwe katika matawi ya miega ili liendelee kukua kuelekea chini. Endapo kuna upepo mkali, marando yafungwe kwenye miega kwa muda ili yasivunjike. Kilimo cha Zao la Vanilla 11

Mchoro Na 3: Jinsi ya kuningíiniza marando 2.6.5 Kulisha Marando Kulisha marando ni kitendo cha kufukia ardhini sehemu ya kipande cha rando ili kiweze kutoa mizizi na kuongeza nguvu ya kuchukua chakula kutoka kwenye udongo. Kazi hii hufanywa baada ya rando lililoningíinizwa kurefuka sana kiasi cha kutambaa ardhini, katika hatua hii mmea huweza kuwa na umri wa miezi sita hadi tisa kutegemea na utunzaji. Jinsi ya Kulisha Ondoa majani matatu hadi manne kwenye rando lililoingíinizwa na kurefuka sana. Fukia kwenye udongo, karibu na shina sehemu iliyoondolewa majani. Weka matandazo katika sehemu iliyofukiwa ili kuhifadhi unyevu. Funga sehemu ya juu ya rando katika mti wa kuegemea ili liendelee kukua. Marando mawili hadi mitatu yalishwe kwa wakati mmoja na mengine yaachwe kwa ajili ya kutoa maua na kupata marando ya kupanda. 12 Kilimo cha Zao la Vanilla

Kumbuka: Kulisha kufanyike wakati wa mvua ili marando yaweze kutoa mizizi kwa urahisi. Kazi hii irudiwe kila wakati ili rando mama litakapokatika machipukizi yake yaendelea kukua. Mchoro Na 4: Jinsi ya kulisha rando 2.6.6. Kusisimua Kusisimua ni kitendo cha kuufanya mmea kuwa katika hali ya kuweza kutoa maua. Kitendo hiki kifanywe wakati mmea ukiwa umefikia umri wa mwaka 1 na nusu au zaidi, na hufanywa wakati wa kiangazi ili kuepuka kupata matawi mengi badala ya vitumba vya maua. Mmea usiosisimuliwa hautoi maua au hutoa maua machache na kusisimua mapema kunaweza kuuchosha mmea. Jinsi ya Kusisimua Chagua matawi matatu hadi matano yanayoningíinia. Kusisimua matawi mengi kunaweza kuudhoofisha mmea au kuzaa maharage madogo. Kata ncha ya rando ili kuwezesha vitumba vya maua kukua na kuwa tayari kufunguka au kutoa maua. Ukataji wa ncha huweza kufanyika kama ifuatavyo: Kukata ncha ndogo (mdomo wa rando) kwa mkono. Hii hufanyika kwa rando fupi linaloningínia. Kilimo cha Zao la Vanilla 13

Kukata rando kwa kisu kikali, kwa rando linaloningínia ambalo halijafikia urefu wa kupanda. Kukata rando kwa kisu kikali kwa rando refu linaloningíinia (lenye urefu wa kuweza kupandwa, sentimita100-150). 2.7 Uchavushaji Ni kitendo cha kuunganisha chavua kutoka katika sehemu dume ya ua na kuweka katika sehemu jike ya ua, hufanyika baada ya maua kuchanua. 2.7.1 Uchanuaji wa Maua Mmea wa Vanilla hutoa maua miezi miwili hadi mitatu baada ya kusisimuliwa. Maua huchanua kwa kipindi cha masaa matatu hadi manne kuanzia saa tatu asubuhi hadi saa saba mchana kwa muda wa miezi miwili hadi mitatu kutegemea unyevu uliopo kwenye udongo na kiwango cha Jua. Ua huchanua kwa muda huo na hudondoka baada ya siku 1 ikiwa halikupata chavua. Hivyo ni muhimu uchavushaji ufanyike kwa haraka na kwa uangalifu mkubwa. Picha Na 4: Ua lililochanua 2.7.2 Jinsi ya Kuchavusha Mmea wa vanilla, ili uweze kutoa matunda inabidi uchavushwe. Ua la vanilla kwa kawaida huchavushwa na nyuki jamii ya melapona ambao hawapo hapa nchini. 14 Kilimo cha Zao la Vanilla

Nyuki hao hupatikana Mexico na katika nchi nyingine za Amerika ya Kati. Hivyo uchavushaji hufanywa kwa mikono kwani umbile la ua haliruhusu nyuki wa aina nyingine kufanya uchavushaji. Uchavushaji hufanywa kwa kufuata hatua zifuatazo: Gawa petali ya ua la vanilla katika sehemu mbili kwa kutumia pini, sindano, au mwiba. Hakikisha vifaa hivyo ni safi. Kunjua sehemu jike ya ua (stigima) kwa kuelekea juu ili kuwezesha kulala sambamba kwenye sehemu dume ya ua (stameni). Unganisha stameni na stigima na kubana taratibu kwa dole gumba kwa nusu dakika ili kuruhusu chavua kuingia kwenye stigima. Ua lililochavushwa vizuri, hubaki likiningíinia kwenye kikonyo chake. Ikiwa uchavushaji haukufanikiwa, ua hudondoka baada ya siku moja au mbili. Kiasi cha maua au mapodo nane hadi 12 yaachwe katika kila kitumba. Aidha vitumba vinne hadi nane viruhusiwe kukua katika kila rando na visizidi 20 kwa mmea. Picha Na 5: Jinsi ya kuchavusha Kilimo cha Zao la Vanilla 15

2.8 Magonjwa, Wadudu na Wanyama Waharibifu Mmea wa vanilla kwa kawaida haushambuliwi mara kwa mara na magonjwa au wadudu waharibifu kama shamba limetunzwa vizuri. Mashambulizi ya magonjwa na wadudu waharibifu ni dalili ya utunzaji duni wa shamba. Ili kuepuka hali hiyo, ni muhimu kukagua shamba kila wakati kubaini na kurekebisha yafuatayo: Nafasi kati ya mmea na mmea ni ya kutosha kuruhusu mzunguko wa hewa safi na hivyo kupunguza hali inayoruhusu vimelea vya magonjwa kuishi na kuzaliana. Kivuli kisiwe kizito ili kuepuka giza linalowavutia wadudu waharibifu na kuruhusu vimelea vya magonjwa. Kivuli chepesi husababisha kuungua kwa majani na kufanya mmea kutokua vizuri Afya ya mmea ikaguliwe kwa makini. Kulisha marando kila mara kunaongeza uwezo wa mizizi kuchukua chakula ardhini hivyo mmea hukua vizuri. Mmea wenye afya nzuri haushambuliwi na magonjwa pia hustamilii mashambulizi ya wadudu waharibifu. 2.8.1 Magonjwa (i) Kuoza kwa Mizizi (Root rot) Ugonjwa huu husababishwa na kuvu inayoitwa Fusarium batatis Woollenw.var.vanillae Tucker. Dalili Mmea kunyauka na majani kuningíinia. Majani kubadilika rangi na kuanza kuwa ya manjano na hatimaye kukauka. Mmea kunyauka sehemu ya chini iliyo kati ya shina na mizizi. Kudhibiti Ondoa maji yaliyotuama. Epuka kujeruhi mizizi. Tumia dawa za ukungu kama Bordeaux mixture 5%. 16 Kilimo cha Zao la Vanilla

(ii) Chule ya Majani, Matunda (Anthracnose) Ugonjwa huu husababishwa na aina ya kuvu inayojulikana kama Calospora vanillae Massee. Dalili Mapodo na majani kuwa na madoa ya rangi ya kahawia. Majani na ncha ya juu ya shina hunyauka. Mizizi na mapodo na hunyauka Mapodo hudondoka Kudhibiti Kuzuia maji yasituame ardhini Kutengeneza kivuli chepesi, Kupunguza matawi Kuzingatia nafasi kati ya mmea na mmea ili kuruhusu hewa safi kupita vizuri. Kunyunyizia dawa aina ya Bordeaux mixture (1%) au Captafol 0.1% kabla ya mimea kuchanua. (iii)ubwiri Vinyoya (Downy mildew) Husababishwa na kuvu aina ya Phytophthora jatrophae Jens ambao hushambulia mti wa Jatropha unaotumika kama muega. Pia hushambulia mapodo yakiwa shambani na baada ya kuvunwa. Dalili Mapodo ya vanilla na majani ya jatropha huwa ukungu mweupe. Kudhibiti Kufuata kanuni bora za utunzaji wa shamba. Kutumia dawa za ukungu kama Nitrophenol 0.5 Kilimo cha Zao la Vanilla 17

2.8.2 Wadudu, Ndege na Wanyama Waharibifu (i) Wadudu Wadudu wanaoweza kushambulia vanilla ni pamoja na katapila na jongoo. Katapila Hukata ncha ya mmea inayokua Kudhibiti Kagua shamba mara kwa mara ili kutambua kuwepo kwa wadudu hao na kuwaua. Jongoo Hukwangua shina na kuacha michubuko Kudhibiti Kagua shamba mara kwa mara na kuwaua. (ii) Ndege Kuku Huharibu mmea kwa kuparura juu ya ardhi na kusababisha kujeruhi na kukata mizizi. Uharibifu huu husababisha mmea kuwa katika mazingira rahisi ya kushambuliwa na vimelea kama Fusarium batatis ambao huozesha mizizi ya mmea. Kudhibiti Zuia kuku wasiingie shambani. (iii) Konokono Husababisha uharibifu zaidi kipindi cha mvua. Wanapotambaa kwenye mmea huacha utando, hasa katika sehemu inayochipua na kusababisha mmea kudumaa. 18 Kilimo cha Zao la Vanilla

Kudhibiti Kagua shamba mara kwa mara na kuwaondoa. Weka mchanganyiko wa mbolea ya samadi na majivu kuzunguka shina la mmea ili kuzuia wasiweze kupanda juu ya mimea. Kilimo cha Zao la Vanilla 19

20 Kilimo cha Zao la Vanilla

SURA YA TATU UVUNAJI Mapodo ya vanilla hukomaa na kuwa tayari kuvunwa baada ya miezi sita hadi tisa tangu maua kuchavushwa. 3.1 Hatua za Kukomaa kwa Vanilla Ukomaaji wa podo (harage la Vanilla) la vanilla hupitia hatua tano zifuatazo: (i) Podo hurefuka na kuwa na rangi ya kijani iliyokolea. (ii) Ncha ya podo hubadilika na kuwa njano. (iii) Rangi ya njano husambaa taratibu katika podo. (iv) Ncha ya podo hubadilika rangi na kuwa ya kahawia (v) Podo hupasuka kuanzia chini. 3.2 Jinsi ya kuvuna Uvunaji wa zao la vanilla huzingatia hatua za ukomaaji wa podo na njia ya ukaushaji itakayotumika. Mapodo huvunwa kwa kukata kikonyo kutumia kisu kidogo. Katika hatua ya kwanza ya ukomaaji, mapodo hayana vanillin ya kutosha hivyo yasivunwe katika hatua hiyo. Mapodo yanaweza kuvunwa yakiwa katika hatua ya pili na ya tatu endapo yatakaushwa kwa njia ya Bourbon. Mapodo yanayokaushwa kwa njia ya kukata na kukausha haraka huvunwa yakiwa katika hatua ya pili, ya tatu na ya nne. Mapodo yasiachwe hadi kufikia hatua ya tano ya ukomaaji kwani ubora wake hupungua. Uvunaji ufanyike kila baada ya siku moja hadi mbili ili kuepuka kupasuka kwa mapodo. Uvunaji huendelea kwa muda wa miezi miwili mfululizo au zaidi kulingana na ukomaaji wa mapodo. Marando yaliyosisimuliwa na kutoa mapodo yakatwe na kuondolewa shambani baada ya kuvunwa. Kilimo cha Zao la Vanilla 21

3.3 Mavuno Mavuno ya zao la vanilla hutofautina kulingana na umri wa mmea na utunzaji wa shamba. Mavuno ya kwanza huanza kati ya miaka miwili na nusu hadi mitatu kwa wastani wa kilo moja sawa na mapodo 50 hadi 60. Mmea unapofikia umri wa miaka minne hadi nane, mavuno huongezeka kufikia kilo tatu hadi tano kwa mmea. Hata hivyo mavuno huweza kupungua mmea unapofikia miaka 15 na kuendelea. Hekta moja ya shamba la vanilla lililotunzwa vizuri hutoa mavuno tani tatu hadi tano za mapodo mabichi sawa na wastani wa kilo 500 hadi 800 za mapodo yaliyokaushwa kwa mwaka. 22 Kilimo cha Zao la Vanilla

SURA YA NNE UKAUSHAJI NA UHIFADHI 4.1 Utangulizi Mapodo ya vanilla hukaushwa kwa njia mbalimbali kulingana na utaalamu unaotumika, vifaa vilivyopo na matakwa ya mnunuzi. Ili kupata ubora unaotakiwa, mapodo yakaushwe mara baada ya kuvunwa. Njia za ukaushaji zinazotumika zaidi ni Bourbon na Mexico. Njia hizi huhitaji uangalifu na utaalamu wa kutosha ili kupata madaraja mbalimbali, ladha, na harufu inayohitajika. Njia zote mbili hupitia katika hatua kuu nne za ukaushaji. Hapa nchini, njia ya ukaushaji inayotumika kwa sasa ni Bourbon. 4.2 Ukaushaji kwa Njia ya Bourbon Njia hii ya ukaushaji huhusisha hatua zifuatazo: 4.2.1 Kuchovya Mapodo kwenye Maji moto (Blanching). Hatua hii huyazuia mapodo yasiendelee kukomaa na kuanza kutoa ladha. Mapodo mabichi hupangwa kulingana na ukubwa na hatua za ukomaaji. Mapodo hayo hupangwa katika mafungu yasiyozidi uzito wa kilo 30 ili kurahisisha uchovyaji. Mapodo huwekwa na kufungwa katika mifuko ya vitambaa maalumu vinavyoruhusu joto la maji kupenyeza kwa urahisi. Mapodo yaliyovunwa katika hatua ya pili, tatu, na nne ya ukomaaji, yatumbukizwe katika maji yenye joto la nyuzi 60 hadi 65 za Sentigredi kwa muda wa dakika tatu hadi tatu na nusu. Mapodo yaliyovunwa katika hatua ya tano ya ukomaaji, yatumbukizwe kwenye maji ya moto kwa muda usiozidi dakika moja. Mapodo yaliyochovywa kwenye maji ya moto vizuri, huwa na rangi ya kijani iliyokolea hadi kahawia. Kilimo cha Zao la Vanilla 23

4.2.2 Kuhifadhi Joto (sweating) Lengo la hatua hii ni kuongeza joto katika mapodo ili kuruhusu vimengíenya (enzymes) kufanya kazi ya kutoa kemikali ya vanillin ambayo huongeza ladha na harufu inayohitajika. Mapodo yaliyochovywa maji moto hutolewa maji na kufungashwa katika vitambaa vyeupe na mablanketi yanayoweza kuhifadhi joto. Mapodo huwekwa kwa muda wa siku moja hadi mbili (saa 24 hadi 48) katika makasha maalumu yanayohifadhi joto. Mapodo hutolewa kwenye makasha baada ya siku moja au mbili na kutandazwa ili kuondoa yasiyo na rangi ya kahawia. Katika hatua hii, mapodo huwa na rangi ya kahawia iliyokolea. 4.2.3 Kukausha Katika hatua hii, mapodo huanikwa asubuhi au jioni wakati jua sio kali. Mapodo yaliyofungashwa kwenye vitambaa vyeupe na mablanketi hutandazwa juu ya vichanja na kuanikwa kwa muda wa saa moja au mbili. Baada ya saa moja au mbili, mapodo hufungashwa tena kwenye mablanketi na kurudishwa ndani. Kazi hii huendelea kwa muda usiopungua wiki tatu. Baada ya wiki tatu, mapodo hutandazwa ndani, juu ya vichanja vinavyoruhusu hewa ya kutosha. Ukaushaji wa ndani huchukua muda wa miezi mawili au mitatu. Ukaguzi ufanywe mara kwa mara ili kuondoa mapodo yenye hitilafu na kutenga yaliyowahi kukauka. 4.2.4 Kuhifadhi Ladha Hii ni hatua ya mwisho katika mtiririko mzima wa ukaushaji. Katika hatua hii, mapodo huwekwa katika makasha maalumu kwa muda wa miezi mitatu hadi mitano ili kuongeza ladha ya vanilla. 24 Kilimo cha Zao la Vanilla

4.3 Kufungasha Vanilla iliyokwisha kaushwa vizuri hufungashwa kulingana na madaraja. Uzito wa kila kifungu na aina ya ufungashaji hutegemea mahitaji ya soko. Kilimo cha Zao la Vanilla 25

26 Kilimo cha Zao la Vanilla